About Breast Cancer - FAQ

FAQ

Mwanamke akiwa na saratani ya matiti yote akipata mimba inakuwaje?

Mwanamke akiwa na saratani ya matiti hata kama ni titi moja tu madaktari wanaangali hali ya ugonjwa, hatua ugonjwa ulipofikia na matibabu atakayopewa mgonjwa. Kuna nyakati madktari watashauri mimba itolewe.

Je ni hatua zipi mwanaume anatumia kujipima?

Mwanaume anatumia njia sawa na zile anazotumia mwanamke kujipima japo yeye hana titi kubwa lakini anaangalia ikiwa kuna uvimbe wowte kwenye eneo la titi na chuchu.

Ufanye nini ili kuepukana na saratani ya matiti?

Kupunguza kutumia au kufanya vitu ambavyo ni vichochezi vinavyochangia kupata saratani ya matiti. Kwa mfano:

  1. Matumizi ya vyakula veynye kemikali
  2. Uvutaji sigara: Kuna matokeo ya tafiti yenye kukinzana kuhusu uhusiano wa uvutaji sigara na hatari ya kupata saratani ya matiti. Baadhi ya tafiti zinaonyesha uhusiano wa karibu kati ya uvutaji sigara na uwezekano wa kupata saratani ya matiti. Tafiti nyinggine zinaonyesha majibu yenye kutofautiana kuhusu uhusiano wa uvutaji wa sigara na saratani ya matiti. Hata hivyo kwa ujumla wanawake wanaojizuia kuvuta sigara wanakuwa na afya njema zaidi kuliko wale wanaovuta sigara.
  3. Unywaji wa pombe kupita kiasi: imeonekana kuwa wanawake wanao kunywa pombe zaidi ya chupa moja kwa siku wana uwezekano wa kupata saratani ya matiti.
  4. Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi; Tafiti zinaonyeshakuwa wananwake wanaopendelea kula vyakula vyenye mafuta mengi na zaidi mafuta ya wanyama, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata huu ugonjwa.
  5. Kutofanya mazoezi kwa wale wanene.

NB: Hizi ni baadhi ya sababu ambazo zinaendana na matakwa ya mwanadamu. Lakini kuna sababu ambazo zipo nje ya uwezo wa mwanadamu kwa mfano:

6. Kuzaliwa mwanamke una hatari kubwa ya kupata saratani ukilinganisha na mwanaume ambao ni asilimia ndogo sana hupata saratani ya matiti.

7. Uzazi: Mwanamke ambaye hajapata Baraka ya mtoto wapo kwenye hatari sana ya kupata saratani ya matiti. Kunyonyesha kunasaidia kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.

8. Umri: Umri nao una uwezekano wa kupata saratani ya matiti kwa maana ya kwamba kadri umri unavyoongezeka ndiyo pia uwezekano wa kupata saratani ya matiti unavyozidi kuwa mkubwa. Wanawake walio na umri wa miaka 50 wapo kwenye hatari kubwa (mara 2 au 3 zaidi) kuliko walio na umri chini ya 45.

9. Familia ambayo ina historia ya kupata saratani ya matiti wanawake toka familia hizi wana hatari ya kupata saratani ya matiti. Wanawake wanaotoka kwenye familia zenye historia ya kuwa na ugonjwa huu wanashauriwa kufuatilia upimaji wa afya zao.

Je ziwa bandia lina madhara?

Ziwa bandia halina madhara yoyote kwa sababu haliunganishwi na mwili.